Tuesday, December 15, 2015

YALIYOJIRI 2015

Tukiwa ukingoni mwa mwaka 2015 kuna watu ambao kupitia mienendo na haiba zao wamenikuza, wamenifunza na wameniwekea misingi ya kujipima kwa namna mbalimbali.
Kupitia maneno yao na matendo yao wamekua taswira ya washauri wa mbali wenye kuleta tofauti kubwa katika jamii yetu.

Watu hawa kwangu wameweka mfano wa kiwango cha juu kukitaraji ama kukifikia katika kukidhi matazamio ya utashi binafsi lakini kwa namna ambayo inajali wale wote wanaokuzunguka.

MWANASIASA WA MWAKA: SEIF SHARRIF HAMAD.

Usipoweza kuufurahia ushindi wako kwa utu, huwezi kupokea kushindwa kwako kwa utu.

Maalim Seif ni mfano wa wanasiasa wachache sana wa kiafrika ambao wameonyesha kuheshimu sana njia ya kidiplomasia katika utatuzi wa migogoro.
Ni mwanasiasa anayejiamini, mwenye msimamo na asiyetetereka lakini amedhihirisha ni kiongozi mwenye staha ya daraja ya juu na muumini wa mazungumzo ya pande mbili zinazokinzana bila kujali mizani ya haki imeegamia upande gani kabla ya shauri husika.

Maalim Seif pamoja na kuwa mshindi halali wa uchaguzi na muathirika wa uamuzi batili wa tume ya uchaguzi bado kwa juhudi binafsi amekua kinara na kichocheo cha mazungumzo ya kutafuta suluhu juu mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar.

MWANAMKE WA MWAKA: MAMA REGINA LOWASA.

Mwanamke bora kwa kiasi kikubwa ndiyo chachu ya familia bora, ndoa bora na jamii bora.

Ushujaa wa sauti ya wanawake katika harakati za ukombozi zilizaliwa upya kutoka katika roho zilizopumzika za wanawake mashujaa kama Bibi Titi Mohammed na Mwamvua Mrisho (aliyekuwa mwenyekiti wa kwanza wa umoja wa wanawake wa Tanu).
Mama Regina alikua sauti ya wanawake walio wengi bila kujali tofauti zao kiitikadi na matabaka yao.
Aliongelea changamoto za kina mama na kuwafikia wakina mama wengi ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza madukuduku yao.
Aliamsha ari kubwa miongoni mwa wanawake na kujenga ushawishi wa ushiriki wa wanawake katika siasa.

Mwaka huu alikua ni alama ng'aavu ya uwezo mkubwa wa wanawake katika kujenga ushawishi ndani ya jamii, alikua ni nuru ya wanawake katika kuzungumzia na kutafuta suluhu ya changamoto zinazoikabili jamii.

Alikua ni nembo ya mke anayeijenga ndoa yake kwa mikono yake, alikua ni kielelezo cha kupigiwa mfano cha mke mwema aliye msaidizi mkuu wa mume wake kama ilivyokua kwa asili ya uumbaji uliotukuka wa Mungu.

Yote haya aliyafanya bila kutetereka huku akitimiza majukumu yake vyema kama mke, mzazi, mlezi, mwalimu jamii na mwanaharakati kisiasa.

HAIBA YA MWAKA:MH EDWARD NGOYAI LOWASSA.

Kuna wakati wa kuongea na kuna wakati wa kukaa kimya, wengi ni wepesi zaidi katika kuongea na wengi zaidi ni wepesi katika kuropoka kwa msukumo wa hisia, lakini wachache sana ni wenye kujua thamani ya kukaa kimya.

Miongoni mwa wachache sana wenye kujua thamani ya kukaa kimya, sijawahi kushuhudia haiba yenye utulivu na staha ya daraja ya juu dhidi ya mihemko yenye joto kali, dhidi ya shutuma zenye kudhalilisha utu katika uasili wake, dhidi ya udhalilishwaji wenye kufedhehesha hata nafsi zilizo pembezoni....sikuwahi kushuhudia hapo kabla.

Sijawahi kushuhudia haiba yenye heshima na utu dhidi ya udhalimu na ufedhuli.
Sijawahi kushuhudia haiba yenye kupiga makasia kwa utulivu wa nafsi na akili ndani ya bahari iliyochafuka yenye mawimbi makubwa ya kuzimisha ndoto, kukatisha tamaa, kuchafua haiba, kuombewa kifo, kuwekewa maneno mdomoni, kuinuliwa vikwazo, kuvikwa nembo ya chuki....sikuwahi kushuhudia hapo kabla.

Lakini mwaka huu nimeshuhudia haiba yenye utulivu, hekima na busara kubwa dhidi ya dhoruba kali ya husda na udhalilishaji wa kupindukia , nimeyashuhudia haya katika haiba iliyosheheni staha katika kiwango cha juu cha kupigiwa mfano kutoka kwa baba yetu Edward Lowasa.

MASHUJAA WA MWAKA: WANAMABADILIKO WOTE NCHINI.

Huwezi kujua unayahitaji mabadiliko kiasi gani mpaka pale unapotambua ni mabadiliko pekee yatakayokuwezesha kujikwamua katika hali ya mtanziko na udumavu uliyopo.

Juhudi za makusudi zinazofanyika na serikali ya sasa ni muitiko wa msukumo wa sauti zilizopazwa kwa kiwango kikubwa cha utambuzi wa wanamabadiliko juu hatima na matamanio yao kama wana wa ardhi.

Kamwe tusisahau umuhimu wa nguvu ya vuguvugu la wanamabadiliko , ushujaa wao katika kupaza sauti ya mabadiliko, na ujasiri wao katika kuonyesha dhamira yao kwa vitendo, imebadili kwa kiwango cha awali (chakuridhisha) upepo wa kisiasa nchini, ikiwemo utendaji na nidhamu ya uwajibikaji.

Mabadiliko haya si utashi wa mtu binafsi au taasisi ya urais, usikosee katika tafakuri ya mantiki pana, mabadiliko haya yanaakisi kishindo kikuu cha sauti za wanamabadiliko, yanaakisi utambuzi na upevu wa fikra zilizoamshwa na wanamabadiliko.

Bila kujali matokeo ya uchaguzi nawiwa kuwatunuku heshima ya juu wanamabadiliko wote waliojitoa kwa hali na mali, kwa akili zao, nguvu zao na muda wao adhimu katika kusimamia na kukipigania kile walichokiamini.

Hakika hamkuiacha Tanzania kama ilivyokuwa awali, kupitia maono na fikra zenu nimejifunza mengi, mmetufunza wengi na hata wale waliowapuuza awali wamejifunza kimyakimya.

Hamasa huzaa matumaini, matumaini huzaa imani, imani huzaa matendo makuu.
Mabadiliko ni safari na safari ndiyo imeanza, hakika TUTAFIKA....hakika YATATIMIA.KITI CHA URAIS KITAYATIMIZA MABADILIKO TULIYOYAHITAJI NA KUYAKOSA KWA MIAKA 50.
HAKUNA NAMNA NYINGINE BALI KUYATIMIZA MABADILIKO IWE KWA KUPENDA AU KUTOKUPENDA.
2020 HAKUNA KUANGALIA USONI.

Thursday, December 10, 2015

Baraza jipya la Mawaziri hili hapa limetangazwa na rais John Magufuli mapema leo.

Mawaziri - George Simbachakene  na Angella Kairuki
Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.
Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira
Waziri - January Makamba
Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina
Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri - Jenista Muhagama
MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri - Mwigulu Nchemba
Naibu Waziri - William Ole Nasha
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani
Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri - Ashantu Kizachi
Wizara ya Nishati na Madini
Waziri - Prof. Mwigalumi Muhongo.
Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.
Wizara ya Katiba na Sheria,
Waziri - Harrison Mwakyembe
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri - Dk. Augustino Mahiga
Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri - Dk. Hussein Mwinyi
Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri - Charles Kitwanga.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri - William Lukuvi
Naibu Waziri - Angelina Mabula
Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani
Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Charles Mwijage.
Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.
Waziri Bado hajapatikana.
Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri - Ummy Mwalim
Naibu Waziri –  Dkt. Hamis Kigwangala
Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri - Nape Nnauye
Naibu Waziri - Anastasia Wambura.
Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa
Naibu  Waziri– Inj. Isack Kamwela

Magazeti 20 ya Tanzania yalivyoamka na habari kubwa leo Dec 10 2015


Ungana na reporter wako Millard Ayo kwenye kupata stori zote kubwa za Tanzania kupitia millardayo.com ambapo utazipata kwenye video na kwenye maandishi pia bila kusahau kila siku kuanzia saa moja asubuhi hapa millardayo.com nakuwekea magazeti yote ya Tanzania na makubwa yaliyoandika.

Kwa muendelezo wa vichwa vya habari bofya hii link  Millard.com

Wednesday, December 09, 2015

Rais Magufuli Atoa Namba yake Ya Simu Kwa Wavuvi…..Awaahidi Mambo Matatu.

Rais John Magufuli leo ameungana na wananchi katika kufanya usafi ambapo akiwa katika eneo la Feri jijini Dar es Salaam, ameweza kuzungumza moja kwa moja na wavuvi wadogo.

Baada ya kusikiliza kwa makini kero zinazowakabili wavuvi hao wadogo akiwa amekaa ndani ya kifaa duni cha kufanyia uvuvi maarufu kama ‘mtumbwi’ usio na mashine, rais Magufuli aliwaahidi wavuvi hao kuzitatua kero hizo.

Kati ya mambo matatu aliyoahidi kuyafanyia kazi kwa haraka ni pamoja na kuondoa masharti kuwa na ‘Fire Extinguisher’ ambapo alieleza kuwa sharti hilo halina mashiko kwa wavuvi hao wadogo wasio na mashine.

“Kwanza maji yenyewe tu ni ‘fire extinguisher’, si moto ukianza unaingia ndani ya maji,” alisema Dk. Magufuli.

Kadhalika, rais aliahidi kuwasaidia wavuvi hao kwa masharti ya kuunda umoja wao ambao utakuwa na viongozi waadilifu wanaofanya kazi kwa maslahi ya wavuvi hao na sio maslahi ya ‘wakubwa’. Alieleza kuwa atalifanyia kazi suala la wavuvi hao kukopesheka na kuwasaidia kuwa na vifaa bora.

Aliongeza kuwa atahakikisha anafuta ushuru kwa wavuvi hao wadogo ili kuwaondolea kero na mzigo wa gharama.

Pia, alisema atahakikisha anaanza kuwasaidia kadiri awezavyo wavuvi wa eneo la Feri kwa kuwa ni majirani zake.

“Katika kudhihirisha ujirani mwema, hayo matatizo nitayabeba.”

Hata hivyo, rais aliwataka wavuvi hao kuhakikisha hawajihusishi na uvuvi haramu wa kutumia sumu na mabomu.

Katika hali ambayo wengi hawakuitegemea, rais Magufuli alimpa mmoja kati ya wawakilishi wa wavuvi hao namba yake ya simu na yeye akachukua namba ya watu wawili kati yao.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya zoezi hilo, Dk. Magufuli aliwashukuru watanzania wote kwa ujumla kwa kuitikia wito wake wa kufanya usafi huku akieleza kuwa hili linapaswa kuwa zoezi endelevu kwani uchafu hauwezi kuisha kwa kufanya usafi mara moja kwa mwaka.

SIKU YA UHURU;LOWASSA AIBUKA NA MABADILIKO HAYA TENA, SOMA HAPA LIVE

ALIYEKUWA Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa,amesema kuwa wakati taifa linasherekea miaka 54 leo hii ni vema watanzania wakaendelea juhudi za kudai mabadiliko yatakayowatoa katika lindi la umasikini

Neymar kashinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Laliga, ila kaweka rekodi ambayo haiwezi kuvunjwa kamwe …

MICHEZO Neymar kashinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi wa Laliga, ila kaweka rekodi ambayo haiwezi kuvunjwa kamwe …  By Rama Mwelondo TZA
onDecember 8, 2015 133SHARES COMMENTS
Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ni tuzo ambayo Ligi nyingi duniani huwa wanayo hata katika Ligi Kuu soka Tanzania bara huwa ipo, December 8 ndio siku ambayo Ligi Kuu Hispania ilitangaza tuzo ya mchezaji bora wa mwezi, Neymar anayekipiga katika klabu ya FC Barcelona ndio mchezaji aliyefanikiwa kutwaa tuzo hiyo kwa mwezi November.
Tuzo ya mchezaji bora wa mwezi ya Neymar inaingia katika rekodi za staa huyo, kwani stori kutoka fcbarcelona.com zinaeleza kuwa Neymar ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa FC Barcelona kuwahi kutwaa tuzo hiyo, rekodi ya Neymar sio tu ya kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya kwanza kwa upande wake ila ni mchezaji wa kwanza wa FC Barcelona kuwahi kutwaa tuzo hiyo rekodi ambayo haiwezi kuvunjwa.

Tuzo hiyo ya mchezaji bora wa mwezi ya Laliga imeanza kutolewa toka msimu wa 2013/2014, hivyo huu ni msimu wake wa tatu toka ianze kutolewa na imetolewa mara 21 hadi sasa, kwa maana hiyo Neymar ambaye ana magoli 14 katika msimamo wa wafungaji wa Ligi Kuu Hispania, ameweka rekodi ambayo haiwezi kuvunjwa kamwe na mchezaji wa FC Barcelona kwani hata mchezaji mwingine wa FC Barcelona akishinda tuzo hiyo Neymar ataendelea kuwa na rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa FC Barcelona kushinda tuzo hiyo

Tuesday, December 08, 2015

KUMBE NAIBU SPIKA WA BUNGE DKT TULIA ALIKUWA MJUMBE WA BODI YA BANDARI, ALIHUSIKA NA UPOTEVU?

HEBU JIKUMBUSHE KATIKA TAARIFA YA UTEUZI WA BODI YA BANDARI JUNI MWAKA HUU
“WAZIRI wa Uchukuzi, Samuel Sitta amefuta uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA) kuanzia jana na kuteua wajumbe wengine wapya nane wanaounda bodi hiyo.
Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Kifungu Namba 6 Kifungu Kidogo cha 2 (b) cha Sheria ya Bandari Namba 17 ya mwaka 2004, kinachompa mamlaka ya kuvunja na kuteua wajumbe wa bodi.
Sitta alitangaza uteuzi huo jijini Tanga jana wakati wa ziara ya kikazi katika Bandari ya Tanga na kisha kuzungumza na wafanyakazi katika Uwanja wa Baraka bandarini hapo.
Alisisitiza kuwa mabadiliko hayo, yametokana na vitendo vya uonevu alivyokuta vikiendelea kufanywa ndani ya TPA.
Wajumbe wapya walioteuliwa ni pamoja na Mhadhiri wa Chuo cha Sheria Tanzania, Dk Tulia Akson, Mhandisi wa Ujenzi, Norplan Consultants, Musa Ally Nyamsingwa, Mtaalamu wa Manunuzi na Mjumbe wa Bodi ya Posta, Donata Mugassa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa EWURA, Haruna Masebu.
Wengine ni Mhandisi wa Elektroniki wa Bodi ya Wahandisi Tanzania, Gema Modu, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dk Francis Michael, Mkurugenzi wa Mipango NSSF, Crescentius Magori na aliyekuwa Mkurugenzi wa Masoko wa TPA, Flavian Kinunda.
“Uteuzi huu unatengua uteuzi wa wajumbe wa sasa wa bodi hiyo kuanzia leo Juni 2, mwaka huu na lengo la uteuzi wa wajumbe hawa ni kuleta tija na ufanisi wa utendaji kazi ndani ya wa Mamlaka”, alisema.
Uteuzi huo umefuta ule wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TPA, uliofanywa Novemba 6, 2012 na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe uliofanywa kwa mujibu wa Kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Bandari na Kifungu 1(2(i)) cha jedwali la kwanza la Sheri ya Bandari ya mwaka 2004.
Waliofutiwa ujumbe wa Bodi ni Dk Jabir Kuwe Bakari, John Ulanga, Caroline Temu, Jaffer Machano, Dk Hildebrand Shayo, Said Salum Sauko, Mhandisi Julius Mamiro na Asha Nasoro.”

MIEZI 6 BAADA YA UTEUZI

Rais wa Tanzania wa awamu ya Tano Dkt.John Pombe Magufuli katika kasi yake ya kutumbua majipu hatimaye,amevunja bodi yote ya Bandari na kutengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi mkuu wa bandari Bw.Awadhi Massawe (Pichani), 
Mwenyekiti wa bodi ya bandari pamoja maofisa 8 wa bandari .Ameagiza wote wawekwe chini ya ulinzi kwa ajili ya uchunguzi Kufuatia kuibuka kwa upotevu wa makontena zaidi 2000 yaliyosababisha serikali kupoteza mabilioni ya fedha.

Rais  pia  amemsimamisha  kazi katibu mkuu wizara ya uchukuzi Bw.Shabani Mwinjaka.

Monday, December 07, 2015

TCRA YAANDAA MFUMO KABAMBE,KUDHIBITI WEZI WA SIMU

 Shirika la  Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA,lipo mbioni kuzindua mfumo wa rajisi wa namba za utambulisho wa simu za kiganjani (CEIR), ambapo mfumo huo unauwezo kuifanya simu iliyo ibiwa,kuupoteza au kuchukuliwa bila ridhaa kutotumika tena.

Watu mbali mbali wametoa maoni kuhusiana na mfumo huo na kuitaka mamlaka ya TCRA kufanya haraka iwezekanavyo ili kutibu kilio cha muda mrefu cha wizi wa simu.

Saturday, December 05, 2015

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na taarifa za kuwepo kwa Programu (Application) ya simu ikijulikana kama SOFTBOX TANZANIA iliyosemekana iko kwenye Google PLAYSTORE.
Ilidaiwa kuwa program (Application) hiyo ya SOFTBOX TANZANIA ilikuwa na uwezo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi.
Kwa yeyote aliyekuwa na nia hiyo ya kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu mwingine alihitajika kulipia fedha kiasi cha Tshs 35,000/= kupitia mitandao ya simu ili kupata namba ya siri kwa ajili ya kuwezesha nia hiyo.
Mamlaka ya Mawasiliano imefanya uchunguzi kubaini kuwepo kwa programu hiyo na ukweli kuhusu uwezo wake wa kufanya kilichodaiwa, ikiwa ni pamoja na kuangalia madhara ya programu hiyo na sheria inasema nini kuhusu suala hili. Baada ya kufanya uchunguzi wa kina, Mamlaka ya Mawasiliano ilibaini na imejiridhisha kuwa program (Application) hiyo haina uwezo huo wa kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi kama ilivyodaiwa.
Aidha Mamlaka imebaini kuwa watengenezaji (Developers) wa programu hiyo walikuwa na nia ya kutapeli na kujipatia fedha hiyo kiasi cha Tshs 35,000/= kwa njia ya udanganyifu wakitumia kivutio cha kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu za watu binafsi.
Programu (Application) nyingine ya aina hiyo iliibuka tena ikiitwa SIMNET Tanzania ikiwa na maelezo kama ya awali.
Wakati Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania pamoja na Jeshi la Polisi wakiendelea na uchunguzi zaidi, tunapenda kuuarifu umma wa Watanzania kuepuka kufanya mambo yafuatayo:
1. Kuvutiwa na matendo yaliyo kinyume na sheria na maadili ya matumizi mazuri ya mawasiliano kama hili la kunasa au kuingilia mazungumzo ya simu, ujumbe mfupi pamoja na mawasiliano ya WhatsApp kutoka kwenye simu ya mtu binafsi. Kit