Wednesday, December 17, 2014

Mbali na vioja vya Solange, Beyonce kathibitisha kuwa yeye nini dada bora


Alichokifanya mwimbaji nyota Beyoncé Knowles-Carter, kwa mdogo wake Solange Knowles, kimeudhihirishia ulimwengu ni kwa kiasi gani yeye ni moja ya ndugu na dada bora.
Kwa mfano ingekuwa Bongo lile noma ambalo alilifanya Solange kwa shemeji yake, Jay Z huenda undugu ungeishia pale kati ya dada mtu na mdogo wake, haijawa hivyo kwa Queen Bey, ameendelea kushow love kubwa kubwa kila kunapokucha.
Maisha yanaendelea poa kwenye familia hiyo, Beyonce ameshaweka dola nyingi sana kuanzia kwenye honeymoon ya mdogo wake ambayo wazee wa udaku wanasema eti vacation ya Solange na Ferguson kule Brazil ni dada Bey ndiye aliyefadhili kila kitu!
Hakuishia hapo, mpya ikufikie kwamba Beyonce amempa Solange zawadi ya safari ndani ya Boti ya kifahari, first class ambayo ina huduma zote muhimu, dada huyo wa nguvu anaamini mdogo wake anastahili kila aina ya zawadi kwa kuwa kampata mume ambaye alikuwa akimhitaji kwa maisha yake yote.
Beyoncé-Solange-Knowles-lounged-boat
Kweli mwenye mkono wa kutoa hupokea pia, Beyonce hana hasara yoyote kwa zawadi hizo kwa Solange, unakumbuka ile shopping iliyomwendea mtoto wa Kelly Rowland? Titan ambaye ni mtoto wa kwanza wa Kelly Rowland, alienjoy zawadi toka kwa shangazi Bey, kitanda very special kilichochorwa jina la mtoto huyo kwa madini ya dhahabu, suti na jacket la leather na pampers za Luis Vuitton, thamani ya vyote sio chini ya dola laki tatu.

No comments:

Post a Comment