Wednesday, September 24, 2014

Kilichosemwa CHADEMA mbele ya Waandishi wa habari.

Chama cha demokrasia na maendeleo {CHADEMA} kimesema Bunge maalumu la katiba na vikao vyake vinavyoendelea hivi sasa havina uhalali wa kukubalika kwa sababu hakuna maridhiano wala muafaka wa kitaifa hivyo limepoteza uhalali wake kwa sababu ya kuvunjwa kwa sheria ambapo pia chama hiki kimemtuhumu Mwenyekiti Samweli Sitta kuwa analiongoza bunge hilo                                                                      kuvunja sheria.
Aliyeyazungumza haya ni naibu katibu mkuu wa Chadema John Mnyika ambae pia ni mbunge wa Ubungo na kuongeza kwamba kilichofanywa juzi na bunge ni kitendo kisichovumilika kwa kuvunja sheria maalumu ya bunge kwa kuruhusu upigwaji wa kura kwa mtu akiwa nje ya bunge.
Kabla ya kumsikiliza kwa mapana hapa chini, nataka nikupe baadhi ya mistari iliyoandikwa na baadhi ya Magazeti ya Tanzania September 23 2014 >>>> #MWANANCHI – Bunge kutuma Ofisa Saudi Arabia kusimamia kura #TanzaniaDAIMA – UKAWA waokoa shilingi bilioni 2.3, ni kutokana na kususia bunge, katibu akiri hazijaombwa Serikalini.

bofya hapa kusilkiliza kilichosemwa na Mnyika..... Chadema

No comments:

Post a Comment