Wednesday, October 08, 2014

MSAMI NA IRENE UWOYA WAMALIZA KUSHOOT FILAMU YAO NCHINI SOUTH AFRICA

Tumezoea kuona filamu za nje kama "Step Up" na "Stomp the yard"  zinazo onesha masuala ya dance lakini kwa mara ya kwanza Msanii wa Bongo movie Irene Uwoya na Msanii wa Bongo Flavour Msami wamefanikiwa kukamilisha filamu yao ya kwanza ikiwa na maudhui kama ya filamu hizo za nje lakini ikihusisha zaidi aina za dance za Afrika ,   Ireneuwoya ndio aliemtambulisha Mpenzi wake Msami kwenye kiwanda cha bongo movie na ndani ya muda mfupi wawili hao tayari wamefanya kitu kikubwa kinachoweza badilisha tasnia nzima ya filamu Tanzania,   Msami alipokua akihojiwa na kipindi cha XXL cha clouds fm alifunguka kuwa filamu hiyo itahusu masuala ya Dance na aliongeza kuwa filamu hiyo imefanyika nchini South Africa na baadhi ya scene zimeigiziwa nchini uturuki pia sura za wakali wengine wa Bongo Movie kama Mzee Majuto zitaonekana ndani ya filamu hiyo. Wapenzi wa Filamu wakae tayari kwa kitu hiki cha tofauti na kipya kutoka kwa Sexylady  Irene Uwoya na Msami baby,

No comments:

Post a Comment