Tuesday, December 29, 2015

Ufisadi mwingine waibuliwa bandarini Dar

Serikali imepoteza jumla ya Sh 48.47bilioni baada ya makontena 11,884 na magari 2,019 kupitishwa badarini Dar es Salaam bila kulipiwa kodi.

Hata hivyo, jumla ya watu saba wanashikiliwa na wengine nane wanatafutwa na Jeshi la Polisi kwa kuhusishwa na ukwepaji kodi huo uliolikosesha taifa mapato.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema ufisadi huo umebainika baada ya serikali kuzifanyia ukaguzi bandari zote za nchi kavu (ICDs) jijini Dar es Salaam.

Akifafanua, Waziri Mbarawa amesema makontena hayo 11,884 yalikuwa na thamani ya Sh 47.4 bilioni wakati magari gari 2019 zenye thamani ya sh 1.07bilioni yalitolewa bandarini pasipo kulipiwa tozo.

Sunday, December 27, 2015

SERIKALI YAAPA KWA HILI JUU YA UMEME WA TANESCO


Waziri MUHONGO amesema kwa sababu nchi inataka kukuza uchumi ikiwemo suala la ujenzi wa viwanda hivyo ni lazima umeme nchini uwe wa uhakika na wa bei nafuu katika maeneo yote nchini mijini na vijijini.
Ameeleza hayo katika Kikao cha Kazi Kati yake na wapiga kura wake kutoka vijijini 68 lengo ni kujadili masuala ya uchumi na maendeleo katika jimbo la MUSOMA Vijijini

Yaliyomkuta Harmonize baada ya kupanda kwenye stage mara ya kwanza Dec 25…(+Video

Dec 25 2015 Msanii Harmonize kutokea Wasafi Classic Baby (WCB) aliandika historia nyingine katika maisha yake ya muziki, ambapo kwa mara ya kwanza alipanda kwenye stage toka aachie hit song ya ‘Aiyola’ Shangwe lilifanyika Tanga, Tanzania.
Licha ya yote, kuna mambo yalitokea na hakuyapenda. Unaweza kubonyeza Play hapa chini kuitazama video yote.



Tuesday, December 22, 2015

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Angella Kairuki amesema

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Utumishi na Utawala Bora, Angella Kairuki amesema waajiri wasitegemee Serikali kuruhusu kuendelea kutoa mikataba kwa watumishi wanaostaafu

Ataka mtu akishastaafu aachie vijana wenye uwezo, sio kuongezewa mkataba wakati kuna wengine wenye uwezo

Serikali imewaonya wamiliki wa shule binafsi wanaondelea kutoza ada ya kujiandikisha pamoja na michango mingine, kuacha mara moja.

Serikali imewaonya wamiliki wa shule binafsi wanaondelea kutoza ada ya kujiandikisha pamoja na michango mingine, kuacha mara moja.

Kuhusu ada elekezi, Serikali imesema itakuwa na kikao na wamiliki wa shule ili kujadiliana ni kiwango gani kitakachofaa na kisichowaumiza wananchi.

Wakati hayo yakiendelea, Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu ya juu, Jonathan S. Mbwamba, ameendelea kusisitiza kuwa wanafunzi wote waliokidhi vigezo vya kupata mikopo watapatiwa mikopo hiyo. Idadi ya wanafunzi wanaopata mikopo imeongezeka kutoka 13,582 hadi 53,032.

Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli kwa hatua ambazo anazichukua,

Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli kwa hatua ambazo anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa Bandari ya Dar

Amesema kuwa ameridhishwa na hatua za Serikali ya Awamu ya Tano ya kudhibiti mianya ya kukwepa kodi, kuondoa uzembe na kupambana na ufisadi Bandarini

Akiwasilisha salamu za pongezi kwa Rais Magufuli baada ya kuchaguliwa kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura alieleza jinsi Rais Kagame alivyofurahishwa na hatua ambazo Serikali imechukua dhidi ya viongozi wa Bandari.

Kwa upande wake, Rais Magufuli alimhakikishia Balozi Kayihura kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Rwanda ili wananchi wa nchi zote mbili waweze kunufaika kimaendeleo.

Dk Magufuli alimuomba Kayihura kumfikishia Rais Kagame salamu za shukrani kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa Rais na kwamba amedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano na Rwanda.

Saturday, December 19, 2015

TAASISI 1,200 DUNIANI ZAMPA TUZO YA AMANI EDWARD LOWASSA


Taasisi 1,200 duniani zitampa aliyekuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa Tuzo ya Amani kutokana na utulivu aliouonyesha kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu.
Akizungumza na Mwananchi kutoka Bukavu, DR Congo, mwenyekiti wa Kamati ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa jamii, Mchungaji William Mwamalanga alisema Lowassa amechaguliwa jana mjini Bukavu na wajumbe 1,400 wa mkutano huo.
Mwamalanga alisema wajumbe wanaohudhuria kongamano la amani wanatoka mataifa ya Ulaya, Marekani, Asia na Afrika kwa kuwashindanisha wanasiasa 1,000 ili kumpata Kiongozi Bora wa Amani mwaka 2015, ambaye anajali na kuangalia maslahi ya jamii badala ya madaraka

WATUMISHI TANESCO 10 WASIMAMISHWA KAZI

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme (Tanesco), Felchesmi Mramba, amewasimamisha kazi maofisa 10 wakiwamo wahasibu waandamizi na mafundi kwa kusababisha upotevu wa mapato zaidi ya Sh.milioni 100.


Hasara hiyo ilitokea katika mfumo wa mita kupitia minara ya simu za mkononi na faini Sh. milioni 198.1 za wateja waliobainika kuiba umeme kwa 

kuchakachua mita zao.
Hata hivyo, shirika hilo limefanikiwa kuokoa fedha hizo zilizotokana na umeme wenye thamani ya Sh. 100,248,386.42 uliotumika bila kulipiwa pamoja na faini kutoka kwa wateja waliojihusisha na wizi wa umeme Sh.
198,105,928.68.
Kadhalika, shirika baada ya kufanya msako mkali limefanikiwa kukamata taasisi binafsi na za serikali pamoja na watu binafsi wakijihusisha na kuhujumu shirika hilo,ikiwemo Shule ya Sekondari ya Jangwani (Sh. 11,023,238.00), Diwani wa Kata ya Sinza C, Joseph Marandu (Sh. 3,443,555.00), Royal Oven Bakery Kawe, (Sh. 4,112,614.00), Havan Hotel, Mbezi Beach (Sh.1,847,913.00) na Kampuni ya Simu ya Viettel Mtwara (Sh. 524,554.76).
Wengine ni, Kampuni ya Saffa Petroleum ya Mkoani Pwani (Sh. 16,105,235.00), Msanii wa Filamu Nchini, Wema Sepetu (Sh. 8,200,496.20) na Kampuni ya Leadcom (Sh. 13,694,632.81).
“Zoezi hili ni endelevu kwa nchi nzima na tutaendelea kuwakamata, kuwatangaza na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wale watakaobainikiwa kulihujumu shirika hatutaogopa wadhifa wala umaarufu wa mtu ama taasisi” alisema Mramba katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Alisema mapema Desemba 6, mwaka huu alitoa taarifa kwa wale wote wanaojihusisha na wizi wa umeme ama wenye mita zenye matatizo, lakini walijisalimisha ni watu 30 na kati ya watu 2,156 waliokaguliwa 138 walikutwa na dosari mbalimbali katika mita zao na walilipishwa faini.
Akifafanua, alisema fedha zinazotakiwa kulipwa ni Sh. milioni 198.1 na zilizokwishalipwa ni Sh. milioni 44.9 wakati waliofikishwa kwenye vyombo vya sheria ni watu 37 kwa makosa mbalimbali. Akizungumzia kuhusu hatua atakazowachukulia watumishi 10 aliowasimamisha kazi, Mramba alisema uchunguzi unaendelea na fedha wanazodaiwa kuzifanyia udanganyifu zitalipwa na kampuni ya simu husika.
Mramba alisema ili kuhakikisha kero za huduma zinamalizika, katika kila ofisi ya kitengo cha dharula kutakuwa na  Ofisa wa huduma kwa wateja na mhandisi ambao watasimamia muda na ubora wa huduma wanazopata wateja baada ya kutoa taarida za dharura.
“Kuanzia sasa kazi ya mafundi inapokamilika maofisa hawa niliowataja watawajibika kuwapigia simu wateja waliotoa taarifa kuhakiki kama kazi zimefanywa kwa wakati na mteja ameridhika … utaratibu huu utaanza leo (jana),” alisema Mramba.

Tuesday, December 15, 2015

Bodi ya mikopo yaagizwa kuwalipa wanafunzi

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi STELLA MANYANYA ameiagiza bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini kuhakikisha


Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi STELLA MANYANYA ameiagiza bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini kuhakikisha wanafunzi walio kwenye orodha ya kupatiwa mikopo wanapewa fedha wanazostahili ifikapo kesho Jumanne ili waweze kuendelea na masomo.
MANYANYA ametoa agizo hilo katika ziara aliyofanya katika bodi hiyo na Tume ya sayansi na teknolojia-COSTECH na Tume ya Vyuo Vikuu –TCU jijini DSM

ALICHOKIBAINI LEMUTUZ KUHUSU DKT MWAKA


STRAIGHT TALK:- Ok guys kama nilivyosema ninarudia tena Dr.Mwaka ni rafiki yangu na ni my Client ni mtumzima mwenye akili timamu sijawahi kuwa na sababu ya kum doubt leo nimemtaka in private anihakikishie kwamba hizi tuhuma si za kweli na AMEFANYA HIVYO amenitumia kila kinachotakiwa Ku prove tofauti na kila anachotuhumiwa.
Nilitaka kujiridhisha na so far nimeridhika ana kila anachotakiwa kuwa nacho kufanya yote anayoyafanya…nilitaka kuweka wazi hilo tu NIMERIDHIKA unless nije niambiwe tofauti again nitasema…again sijawahi kumkimbia rafiki akiwa kwenye matatizo NEVER…in my life huwa sijibizani na yoyote anayemuhusu ndugu yangu wa damu NEVER maana nitakuwa namvunjia heshima anayemuhusu na siwezi kugombana na damu yangu kwa sababu ya MTU wa kupita hapana.
Sasa imebaki Naibu Waziri  na again ninamtakia heri na niaamini UKWELI UTAJULIKANA WOTE TUTAKUWA HURU makosa ni kumuhukumu MTU bila FACTS just because Fulani kasema kama ushahidi WOTE alionipa Dr. Mwaka ni wa kweli basi TUTAKUWA na aibu ya the Century by leo jioni