Friday, December 04, 2015

Huduma ya Paypal Tanzania

Malipo kwa njia ya PAYPAL; Hii ni njia au huduma nzuri sana na ya haraka kulipwa au kulipa hela. Ni huduma inayotumika sana Duniani kwa sasa. Lakini nchi yetu ya Tanzania hususan Benki kuu wamekataa malipo ya huduma hii yaani mtu, taasisi au shirika haliwezi kulipa mtu, taasisi au shirika kwa kutumia PayPal. Tanzania inaruhusu tu kulipa kwa kutumia Pay Pal lakini hairuhusu kulipwa, hii ni ajabu sana kwani nchi yetu inahitaji hela za kigeni kila uchao lakini hairuhusu huduma nzuri na ya haraka ya kuleta hizo fedha za kigeni. 

Majirani zetu Wakenya wanaruhusu kulipa na kulipwa kwa kutumia PAYPAL, 
nauliza; sisi Tanzania ni Kisiwa? 

Naomba mamlaka husika husasan benki kuu waangalia namna ya kuruhusu huduma hii Tanzania. NAWASILISHA

souce:              Jamii forum

No comments:

Post a Comment