Kamishna anayesimamia mipango miji Lagos, Olutoyin Ayinde amesema uchunguzi uliofanywa na tume iliyoongozwa na Oyetade Komolafe umeonyesha hakuna kibali kilichotolewa na mamlaka hiyo kuidhinisha ujenzi wa jengo la ghorofa sita.

Anyinde amesema mamlaka hiyo imeagiza mamlaka ya anga kuchunguza juu ya ndege ambayo imedaiwa kuzunguka jengo hilo muda mfupi kabla ya jengo kuanguka.
Kesi hiyo inayosikilizwa mahakama kuu Lagos imeahirishwa mpaka Novemba 5 ambapo T.B Joshua atatoa ushahidi. Jengo hilo lilianguka Septemba 12 na kuua watu 116.
No comments:
Post a Comment