Friday, October 17, 2014

Tuhuma nzito kwa Abbas Mtemvu mbunge wa Temeke ccm

 Abbas  Mtemvu ambaye ni mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CCM anadaiwa kutumia mbinu chafu ili binti yake aitwaye Sitti Abbas aweze kuipatia umaarufu taasisi yake ijulikanayo kama 'Mtemvu foundation' yenye ofisi zake kuu maeneo ya Mbezi beach Dar es Salaam, taarifa mbalimbali zimebainisha.

Abbas Mtemvu amedaiwa kuchukua fedha za mfuko wa jimbo la Temeke takribani shilingi milioni 65 ambazo alidai ni za kuisaidia taasisi yake hiyo ya 'Mtemvu foundation' ambayo inajinasibu kama taasisi inayosaidia watoto wasiojiweza ili kuzihonga kamati za miss Chang'ombe mwaka 2014-15, miss Temeke mwaka 2014-15 na ile ya miss Tanzania mwaka 2014-15 kwa lengo la kumpitisha binti yake huyo ajulikanaye kama Sitti ambaye alikuwa akiishi Marekani ili kutwaa mataji hayo.

Aidha kamati zote zilisimamiwa na Hasheem Lundenga ambaye alitakiwa kuhakikisha binti huyo wa Mtemvu ananyakuwa mataji hayo.Hasheem Lundenga ndiye muasisi na mwenyekiti wa kamati inayoandaa na kuratibu shughuli zote za kumsaka miss Tanzania.

Binti huyo wa Abbas Mtemvu (Sitti Abbas) ambaye ana umri wa miaka 29, alizaliwa mnamo mwezi wa tano mwaka 1985 kama alivyothibitisha mama yake mzazi na hivyo moja kwa moja kukosa sifa za kushiriki mashindano hayo.

Hata hivyo hali hiyo imepewa msukumo na Abbas akitumia fedha ili binti yake huyo aitangaze taasisi yake hiyo ya Mtemvu foundation kimataifa huku akijua kuwa binti yake hakuwa na sifa za kushiriki mashindano hayo kutokana na kigezo cha umri ambapo inatakiwa mshiriki asizidi miaka 24.

Hata hivyo katika mashindano hayo binti huyo wa Mtemvu alidai kuwa ana umri wa miaka 18 na ana shahada ya uzamili (masters) jambo ambalo lilipingwa vikali na MAMA YAKE MZAZI ambaye alithibitisha kuwa mwanaye alidanganya umri kwa kupunguza takribani miaka 11.Sitti Abbas ndiye aliibuka mshindi wa mataji ya miss Chang'ombe, miss Temeke na miss Tanzania mwaka 2014-15 hivyo kutimiza ndoto za baba yake ambaye ni Abbas Mtemvu mbunge wa Temeke kwa tiketi ya CCM za kuitangaza taasisi ya Mtemvu foundation katika ngazi ya kimataifa kama alivyotarajia.

No comments:

Post a Comment