Wednesday, October 15, 2014

Ujerumani nayo imeingia kwenye headlines za Ebola, wa kwanza amefariki.

Mfanyakazi wa Umoja wa mataifa aliesafirishwa mpaka Ujerumani akitokea Liberia wiki iliyopita baada ya kupatwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola, amefariki dunia kwenye hospitali ya St. Georg Ujerumani.
Kifo chake kinamfanya kuwa binadamu wa kwanza kufariki kwa Ebola ndani ya ardhi ya Ujerumani ambapo Mwanaume huyu raia wa Sudan mwenye umri wa miaka 56 alifikishwa kwenye hospitali hiyo akiwa na hali mbaya ambapo amefariki jana usiku baada ya hali yake kuwa mbaya pamoja na kwamba alipewa uangalizi mkubwa wa kupatiwa matibabu.
Kuna hii stori ya shirika la afya la umoja wa mataifa kwamba karibu watu 8,400 waliathirika na gonjwa la ebola ambapo 4,000 kati yao wamefariki.
Msudan huyu aliefariki dunia anakuwa mgonjwa wa tatu wa Ebola kutibiwa nchini Ujerumani sababu tayari kuna Mganda mmoja daktari amekua akitibiwa huko Frankfurt, wakati Yule Msenegal aliruhusiwa kutoka hospitali hivi karibuni baada ya kutibiwa kwa wiki tano.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza 

No comments:

Post a Comment