Tuesday, December 22, 2015

Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli kwa hatua ambazo anazichukua,

Rais Paul Kagame wa Rwanda amempongeza Rais John Magufuli kwa hatua ambazo anazichukua, hasa katika usimamizi na utendaji kazi wa Bandari ya Dar

Amesema kuwa ameridhishwa na hatua za Serikali ya Awamu ya Tano ya kudhibiti mianya ya kukwepa kodi, kuondoa uzembe na kupambana na ufisadi Bandarini

Akiwasilisha salamu za pongezi kwa Rais Magufuli baada ya kuchaguliwa kuongoza Serikali ya Awamu ya Tano Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Balozi wa Rwanda nchini, Eugene Kayihura alieleza jinsi Rais Kagame alivyofurahishwa na hatua ambazo Serikali imechukua dhidi ya viongozi wa Bandari.

Kwa upande wake, Rais Magufuli alimhakikishia Balozi Kayihura kuwa Serikali yake itaendelea kushirikiana na Rwanda ili wananchi wa nchi zote mbili waweze kunufaika kimaendeleo.

Dk Magufuli alimuomba Kayihura kumfikishia Rais Kagame salamu za shukrani kwa kumpongeza kuchaguliwa kuwa Rais na kwamba amedhamiria kuimarisha zaidi ushirikiano na Rwanda.

No comments:

Post a Comment